|
|---|
|
|
Sawa! Awali Kanisa lilikataa kuwapa daraja la upadre
wanawake. |
![]() |
![]() |
Upendeleo wa aina tatu uliwazuia wanawake kutokufanya shughuli
za kikuhani. 1. Wanawake walichukuliwa kuwa wa chini katika myanja zote: kimaumbile, kiakili na kihisia. Kwa kuwa iliaminika kwamba ni mbegu za kiume tu 'zilizokuwa' na mtoto mtarajiwa,wanawake walichukuliwa kama viumbe visivyokamili. Kwa kifupi wanawake walichukuliw kuwa duni.. 2. Kwa kuwa Hawa alisababisha mwanadamu kupoteza neema, kila mwanamke alidhaniwa kuwa amebeba laana ya dhambi yake. Manawake walichukuliwa kama viumbe wenye dhambi. 3. Watu walidhani kuwa hedhi ya mwanamke humfanya najisi. Kama viumbe najisi, wanawake walitengwa wasikaribie madhabahu na ibada takatifu. |
| Kanisa
lahitaji daima kujikomboa lenyewe kutoka kwenye upendeleo wa kijamii na
kitamaduni unaodhuru mafundisho na maisha yake. Hadi mwaka 1854, mapapa walifundisha kwamba Mungu aliruhusu utumwa, jambo ambolo kwa sasa haliruhusiwi kabisa na Kanisa. Kanisa limefanya makosa mengi ya namna hiyo hiyo wakati wote katika historia yake. Leo hii wanawake wanahitaji kukombolewa kutoka kwenyeupendeleo wa mafundisho ya kanisa ambao bado yanawazuia kushiriki katika shughuli za kikuhani ambazo ni zao katika mpango wa kweli wa Mungu. |
||
| 1 | 2 | 3 | 4 | 5 | 6 | 7 |
| baptised | empowered | liberated | ordained | affirmed | supported | called |
![]() |
|
|
|---|
![]() |
|---|