Kuna walau sababu saba Kwa nini
wanawake wanaweza na yawapasa kepewa madaraja matakatifu.
1.Ukuhani mmoja katika Kristu,
Kwa njia ya ubatizo wanawake na wanaume wanashiriki sawa katika ukuhani mpya wa Kristu. Hii inajumuisha utayari wao katika madaraja matakatifu. click!
2.Wamewezeshwa kuadhimisha
Wakati wa Karamu ya mwisho Yesu aliwawezesha wanawake na wanaume. Wote wanaweza kupewa daraja na kuadhimisha Ekaristi.
click!

3.Upendeleo wa Kiutamaduni
Desturi ya Kanisa ya kutowapa daraja wanawake kama makuhani ililenga
vigezo vitatu vya upendeleo dhidi ya wanawake. Hii iliathiri maamuzi ya viongozi wa Kanisa.click!
4. Wanawake walishawahi kuwa Mashemasi
Mpaka walau karne ya tisa Kanisa liliwapa wanawake sakramenti
kamili ya daraja la ushemasi. Hii inathibitisha kuwa wanawake wanaweza kupewa daraja la upadre click!
5. Uwezo wa wanawake kupewa daraja umekuwapo kwenye mapokeo ya Kanisa yasiyoridhiwa.
Mfano mmojawapo ni ibada ya zamani kwa Maria kama kuhani. Hii
inaonesha kwamba kulingana na hali ya waamini kwa Maria kizuizi dhidi ya wanawake kimeshaondolewa.click!
6. Sehemu kubwa ya Kanisa hukubali daraja la upadre kwa wanawake.
Baada ya sala na utafiti wa ndani, makanisa mengine ya Kikristu sasa
yanawapa wanawake daraja la upadre. Ijapokuwa si kila kitu ambacho makanisa mengine yanafanya chaweza kukubaliwa na Kanisa Katoliki,makubaliano haya ya pamoja ya waamini wa Kikristu yadhihirisha kwamba, daraja kwa wanawake ni kulingana na mtizamo wa Kristu. click!
7. Wanawake pia,kwa hakika, wameitwa kuwa makuhani.
Ukweli kwamba wanawake wengi wawajibikaji wa Kikatoliki huamua
wenyewe wito wa upadre ni ishara ya Roho Mtakatifu ambayo hatuwezi kuipuuza.click!
Hitimisho: Hakuna hoja halali dhidi ya wanawake mapadre, na hamna hoja nyingi za Kikatoliki zinazounga mkono jambo hili.
![]() | Then what about papal teaching banning women priests? Read our frequently asked questions! |

